Mshambuliaji wa pembeni (winga) wa Real madrid Angel Di maria amelia na kilabu yake baada ya kuzuka uvumi kuwa anataka kuuzwa kwenye klabu ya soka ya nchini Uingereza ya Tottenham.
"Inaumiza sana kama mchezaji siku zote unajitahidi kufanya uwezavyo kuisadia kilabu yako lakini mwisho wa siku unasikia kwamba kunampango wakuuzwa Tottnham". alilalamika Di maria wakati akizungumza na Gazeti la Marca.
Di maria kwa sasa ni mchezaji aliye katika kiwango cha juu kutokana na kuonyesha uwezo wake katika michezo mbali mbali ya Real Madrid ukiwemo dhidi ya wapinzani wao Barcelona na ule wa fainali ya ligi ya mabingwa ulaya yaani UEFA.
Msimu iliopita alikua ni mchezaji aliyetegemewa kuhama Real Madrid lakini mwisho wa siku hakuwa yeye kwani tulishudia kuhama kwa mchezaji Mesuit Ozil kuelekea Arsenal na Di maria akibaki kikosini,.
Di Maria amebaki kusema kuwa mstakabali wa maisha yake ndani ya Santiago Bernabeu upo chini ya Real Madrid, endapo wataendelea kumhitaji na kumtumia kama mchezaji wao ama watahamua kumuuza.
"Nilizungumza na kocha nikamweleza nahitaji kuendelea kuwepo pia na yeye alisema ananihitaji uwepo wangu, aliniambia ananitegemea sasa kazi ilibaki kwangu kama mchezaji". alisisitiza Di maria.
Pia Di maria akusita kumsifia kocha wake Ancheloti nakusema kuwa, kajifunza mengi chini ya ualimu wake na alifanya maamuzi sahihi kuendelea kubaki ndani ya Real Madrid.
Alisisitiza kuwa afikilii baadae yake kwa sasa kwani ipo chini ya kilabu yake ya Real Madrid licha ya kukubali uwepo wa timu kubwa zinazo muhitaji lakini awezi sema chochote akisubiri kilabu kusema kama inahitaji aendelee kuwepo ama aondoke.

No comments:
Post a Comment