Sunday, 27 July 2014

LIVERPOOL YAMSAJILI DEJAN LOVREN KUTOKA SOUTHAMPTON

Klabu ya soka ya liverpool imekamilisha usajili wa beki wa kati kutoka Southampton Dejan Lovren.

Lovren amehamia liverpool kwa ada ya uhamisho kiasi cha paundi 20 millioni na kuwa beki wakwanza kikosini hapo kusajiliwa kwa gharama kubwa.

Beki huyo ametoa rekodi ndogo iliyowekwa na Mamadou Sakho beki aliyesajiliwa kwa paundi 18 millioni na sasa lovren ndo beki ghali katika historia ya Liverpool.

Uhamisho huu umekamilisha idadi ya wachezaji watatu msimu huu waliohama Southampton na kutimkia Liverpool akijiunga na wenzie Adam Lallana na Rickie Lambert.

Kwa upande wake Lovren amesema ni furaha kujiunga na klabu kubwa katika historia ya soka Uingereza na ndoto yake imetimia ya kucheza chini ya mashabiki wenye hali na moli wa kushangilia.

Brenden Rogers amesema usajili huu ni kuimarisha safu yake ya ulinzi msimu huu lakni pia ni mchezaji mwenye malengo na uongozi mzuri kwa wenzie awapo uwanjani.

source: LFCTV

Tuesday, 22 July 2014

BRAZIL IMEMTEUA DUNGA KUWA KOCHA MPYA WA TIMU YA TAIFA

Brazil imempa kibarua Dunga cha kukinoa kikosi cha timu ya taifa kuziba nafasi ya kocha Scorali aliyejuzulu.

Dunga mwenye umri wa miaka 50 aliweza kuiongoza Brazil kuchukua kombe la Dunia mnamo mwaka 1994 akiwa kama timu kapteni.

Alikinoa kikosi hicho kwenye mashindano ya kombe la Dunia mwaka 2010 huko nchini Afrika ya Kusini na akatimuliwa kibarua hicho baada ya kuondolewa katika mashindano hayo na timu ya taifa ya Uholanzi kwenye hatua ya robo fainali.

Scorali pia alijiuzulu kukinoa kikoso hicho baada ya kuondolewa kama mwenyeji kwenye mashindano ya kombe la Dunia kama mwenyeji kwa kufungwa goli 7-1 na Ujerumani mabingwa wa mwaka huu.

Dunga kapewa kikosi hicho kwa imani kubwa ya kuleta mabadiliko na kuizoea timu mapema kwa muda mrefu iliwaweze kuja fanya mabadiliko baadae.

MADRID IMEKAMILISHA UHAMIMISHO WA MCHEZAJI JAMES RODRIGUEZ

Klabu ya soka ya Mdrid imefanikisha kumsajili mchezaji wa timu ya taifa ya Colombia na klabu ya Monaco James Rodriguez.

Madrid imekamilisha uhamisho wa Rodriguez kwa ada ya paundi milioni 68 kutoka klabu yake ya Monaco  aliyo iwezesha kucheza UEFA.

Nyota huyo wa Colombia aliweza kung'aa zaidi katika mashindano ya kombe la Dunia yaliyo malizika huko nchini Brazil wiki chache zilizopita.

Rodriguez mwenye umri wa miaka 23 sasa atajiunga na mastaa wa soka wa klabu ya Madrid yaani Ronaldo, Bale, Benzema na wengine wengi.

Klabu yake ya Monaco imetoa shukurani za dhati kwa mchezaji huyo aliyeweza kufunga magoli tisa na kutoa pasi za magori 12.

Amesaini mkataba wa miaka sita ndani ya klabu ya Madrid ya huko Uhispania.

Monday, 21 July 2014

STEVEN GERALD ATANGAZA KUSTAAFU

Kapteni wa timu ya taifa ya Uingereza Steven Gerald ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa.

Steven Gerald amefikia uamuzi huo baada ya haya mashindano ya kombe la Dunia huko nchini Brazil kupita.

Ametoa shukrani za dhati kwa mashabiki wa timu ya taifa na makocha wote aliofanya nao kazi chini ya timu ya taifa.

Gerald amesema sasa anaelekeza juhudi zote kwenye klabu yake ya Liverpool ambayo sasa imefuzu tayari mashindano ya UEFA.

Hakusita kumshukuru kocha Roy Hudgson ambaye alimpa mamlaka ya ukapteni wa timu ya taifa tangu apewe timu hiyo nakusema ameifanya ndoto yake ya utotoni kutimia.

Gerald amemalizia kwa kisema kustaafu kwake majukumu ya timu taifa haimanishi anaitelekeza timu hiyo bali tabaki kufaya kazi na shirikisho la soka nchini humo yaani FA.

ROONEY APANAIA KUMSHANGAZA KOCHA WAKE VAN GAL

Mchezaji wa klabu ya soka ya Manchester United Wayne Rooney  amesema yupo tayari kumshangaza kocha wake mpya Van gal baada ya kuanza kufanya nae mazoezi.

Rooney amesema yupo tayari kufanya kila awezalo mazoezini ili kumuonesha uwezo wake kocha huyo mpya kutoka nchini Uholanzi.

Van gal anatarajiwa kutangaza kapteni wake klabuni hapo wakati wowote ambapo macho mengi yakiwa ni kwa Van persie ama Rooney.

Van persie amekua kepteni wa timu ya taifa chini ya kocha huyo huyo mholanzi ambaye amekifikisha kikosi nafasi ya tatu katika mashindano yaliyokamilika ya kombe la Dunia huko nchini Brazil.

Rooney pia anapewa nafasi kubwa kutokana na ukweli kuwa amekuwa na ushawishi mkubwa ndani ya klabu hiyo na nikiongozi mzuri wa wachezaji wenzake.

Rooney amesema huu ndo wakati wa kumuonesha kocha kile walichonacho wachezaji ili kumrahisishia upangaji wa kikosi cha Man U.

Wachezaji wengine pia kama Mata wanasema wamejiandaa vizuri kutetea klabu ya licha ya kuwa na matokeo magumu katika timu ya taifa iliyoondolewa mapema kwenye mashindano ya kombe la Dunia huko Brazil.

ISCO WENDA AKAHAMIA LIVERPOOL

Mshambuliaji wa kilabu la Real Madrid ya Uhisipania Isco wenda akahamia nchini Uingereza kwenye klabu ya soka ya Liverpool

Taarifa za awali zinasema kuwa liverpool wanajipanga kutuma ofa ya kumsajili mshambuliaji huyo ili kuziba mwanya ulioachwa na mshambuliaji Luis Suarez ailyesajiliwa Barcelona.

Liverpool wametenga kiasi cha paundi milioni 80 kuweza kusajili wachezaji wanao fikiliwa kuwa mbadala wa Suarez.

Kwa upande wake Isco wenda akavutiwa na ofa hii kutokana na ukweli kwamba yeye ndiye atakua mshambuliaji wa mwisho tofauti na Real Madrid anakocheza nyuma ya Mshambuliaji.

Isco ameweza kucheza mechi kadhaa chini ya kikosi cha kocha Carlo Ancheloti licha ya kuwa hana namba ya kudumu kwenye kikosi hicho.

Liverpool wamekuwa wakiaswa kutorudia makosa yaliyo igharimu klabu ya Tottenham baada ya kumuuza Gareth Bale na kukosa mbadala wake yasije tokea pia kwa Liverpool kwa kumuuza Suarez.

Thursday, 12 June 2014

KITAZAME KIKOSI CHA BRAZIL KINACHOANZA LEO DHIDI YA CROATIA

Leo ndo leo ufunguzi wa kombe la Dunia ndani ya nchi ya Brazil ambapo tutawashudia wenyeji Brazil wawaalika Croatia kufungua rasmi michuano hiyo. Mechi hiyo inakadiliwa kuchezwa mishale ya saa 5 usiku kwa saa za Afrika Mashariki

MTAZAME RONADIHNO FEKI ALIYEVAMIA MAZOEZI YA ARGENTINA ILI KUMUONA MESSI

Huyu ndiye Ronadihno feki aliyevamia mazoezi ya timu ya taifa ya Argentina ili kumuona Lionel Messi, shabiki huyo anae fanana kupitiliza na Ronadihno alitokea kusiko julikana na kuwaadaa walinzi kama Ronadinho kwa kuingia uwanjani kwa mbio kumfuata Messi.

Alipomfikia Messi alibidi Messi ashangae na kumuuliza Ronadinho feki kwa nini amefikia uamuzi huo kwa sababu akiitaji kuonana nae hana haja ya kufanya hivyo, alipofika kwa Messi na kumpa mkono, alimshangaza zaidi pale alipo mpigia magoti.

Alopotolewa na wanausalama na kuhojiwa alisema hakuwa na jinsi nyingine ya kumuona messi na kumuonesha jinsi gani anamkubali zaidi ya hiyo ya kutumia nafasi ya ufanano wake na Ronadihno kutimiza ndoto zake.

Kwa upande wake mwssi alibaki kuduwaa na kumshangaa mtu huyo mwisho wake aliishia kumfurahia, Argentina ndio timu inayopata washabiki wengi mazoezini wanaotazama uwezo wa wachezaji hao.

Alipoulizwa ni mchezaji gani mwingine anampenda kiasi hicho ni nani hakusita kumtaja pacha wake wa bandia yaani Ronadinho.

Wednesday, 11 June 2014

BABA WA YAHAYA TOURE ATHIBITISHA MWANAE KUENDELEA KUWEPO MAN CITTY

Baba wa mchezaji wa Man City Yahaya Toure amethibitisha kuwa mwanae ataendela kubaki ndani ya klabu hiyo kutokamna na uvumi uliojitokeza kwamba angeondoka klabuni hapo kutokana na kutothaminiwa licha ya uwezo alioonesha klabini hapo.

Klabu ya Ufaransa ya PSG walionesha nia mamepema nia ya kumhitaji mchezaji huyo ambaye kwa sasa ameonekana kuwa na uwezo mkubwa baada ya kuisaidia klabu yake kubeba ubingwa wa soka nchini Uingereza.

Yahaya Tuoure alitegemewa kuondoka klabuni hapo kutokana na maneno yaliyokuwa yakitolewa na wakala wake kwamba angeondoka kutokana na kutothaminiwa na uongozi wa juu wa klabu hiyo ya Man City.

Baba mzazi huyo aliendelea kusema mwanae ni mtu ambaye huwa hafurahi kuwa kwenye mazingira magumu kwake au yasiyo mpendeza, alisema anamini hayo yatamalizika na mwanae ataendelea kufurahia maisha yake ndani ya ETIHAD.

HAKUNA MIUJIZA KATIKA MAFANIKIO YA SOKA - MWENYEKITI MBEYA CITY

Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Mbeya City Bw Musa Mapunda amesma hakuna miujiza siku zote katika mchezo wa mpira wa miguu. aliyasema hayo kufuatia mafanikio makubwa waliyoyapata klabu ya Mbeya City kwenye ligi ya Tanzania Bara mwaka 2013/2014, licha ya kutobeba ubingwa.

Mbeya City ni klabu iliyopanda daraja msimu uliopita nakufanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu ya ligu kuu ya Tanzania bara, na kuzipiku timu kubwa kama Simba, Kagera sugar na Mtibwa.

Alisema Mpira wa miguu hauna miujiza zaidi ya uongozi mzuri na wenye malengo ya mafanikio ndani ya klabu na kubeza timu kubwa kuwa migogoro wliyonayo ndani ya vilabu vyao ndo chanzo cha timu timu hizo kubwa kuvurunda kisoka.

Aliendelea kusema kuwa kinacho tokea hivi sasa ni watu wenye uchu na madaraka kugombea nafasi ndani ya vilabu vyao ili kutimiza malengo yao binafsi bila kujali maslahi ya timu, kitu ambacho ni makosa makubwa kwa mwenendo wa soka la timu na taifa kwa ujumla.

Kwa sasa Mbeya City wamepata uzamini mkubwa toka kampuni ya kuuza matairi ya magari ya Binslum, Ambayo inakadiliwa kuweka kiasi cha shilingi milioni 360 kwenye mkataba wa udhamini kati ya kmpuni hiyo yenye makazi yake jijini Dar es salaam na klabu hiyo ya jijini Mbeya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa Mbeya City aliendelea kusema kuwa soka ni biashara na ili ufanikiwe unahitaji kuwekeza kiasi kikubwa na kusema timu yao inajipanga vizuri kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

Tuesday, 10 June 2014

VITAZAME BAADHI YAVITUKO MPIRANI VUNJA MBAVU HAPA

YATAZAME BAADHI YA MAGOLI MAZURI YA LUIS SUAREZ YA MWAKA 2014

RONALDO AKILI MESSI KUWA BORA HATA BILA KUBEBA KOMBE LA DUNIA

Mkongwe wa soka nchini Brazil Ronaldo De Lima amekili kuwa mshambuliaji wa Argentina na klabu ya soka ya Barcelona Lionel Messi kuwa bora kama mchezaji wa Dunia hata kama hatapata mafanikio makubwa kwenye kombe la Dunia nchini Brazil.

Mshindi mara nne wa tuzo ya soka ya Dunia (Ballon D'Or) Lionel Messi amekua akipokea sifa kadha wa kadha kutoka kila upande Duniani kwa staili yake ya uchezaji mpira anayewavutia walo wengi, ndani ya umri wake wa miaka 26.

Licha ya kumsifia Ronaldo, alisema kuwa bado ana umri mdogo na anuwezo wa kufanya makubwa zaidi kwenye soka kuliko haya tunayoshuhudia sasa, kwa upande mwingine Ronaldo alipinga Messi kuitwa Mungu wa mpira akisema kuwa bado anahitaji kuonyesha uwezo zaidi ya huu alionaosasa kuitwa hilo jina.

Kwa upande mwingine hakuacha kumtaja wajina wake Mreno Christian Ronaldo nakusema kuwa ni mchezaji mzuri alistaili kuchukua tuzo ya Dunia iliyopita kwani alionyesha uwezo, lakini pia amekuwa akiwafurahisha  wale mashabiki wa Real Madrid kama yeye kwa kuisadia timu kufanya vizuri.

MAN U KUMLIPA LUKE SHAW PAUNDI 160,000 KWA WIKI KAMA MSHARA

Man U wamefikia makubaliano binafsi na mchezaji Luke Shaw wa Southampton kwa kukubaliana kumlipa mshahara wa kiasi cha paundi 160,000 endapo watafanikiwa kupata saini yake kama mchezaji wao.

Beki huyo ambaye atatimiza miaka 19 mwezi ujao wa saba, endapo atajiunga na Man U na kupewa kiasi hicho cha fedha atakuwa ndo mchezaji kinda (mwenye umri mdogo) Duniani kulipwa mshahara mrefu.

kwa hofa hiyo Man U  watakaua wamewapiku Chelsea ambao nao walimwandalia donge nono mchezaji huyo. Morihno alivutiwa na beki huyo wa pembeni akimhitaji kuziba mwnya wa Ashley Cole ambaye anonekana kutokuwa mvuto tena kwake.

United wamekwisha andaa kiasi cha paundi millioni 27 kwa ajili ya Southamton kama dau la kumsajilia mchezaji huyo.

Southampton wanonekan kuwa wagumu kutoa mchezaji wao kwa sasa wakisubiri mpaka aptikane kocha mpya wa kukinoa kikosi hicho kufuatia aliyekuwa kocha wao kupewa kibarua na Tottnham kuziba nafasi ya kocha aliyeondoka.

Monday, 9 June 2014

HATIMA YA WAMBURA NDANI YA UCHAGUZI WA SIMBA KUJULIKANA LEO

Hatima ya Wambura kugombea uraisi ndani ya klabu ya simba kujulikana leo baada ya tume ya rufaa ya TFF kukutana leo kujadili rufaa yake aliyoipeleka mahakamani kupinga kuzuiwa kugombea uraisi ndani ya klabu ya simba.

kamati ya uchaguzi ya simba chini ya mwenyekiti wake Damas Ndumbaro walifikia uamuzi wa kumsimamisha Michael Wambura kama mgombea wa uraisi wakidai kuwa haukuwa na uanachama hai ndani ya klabu.

Baada ya wambura kusimamishwa alifikia uamuzi wa kukata rufaa ndani ya kamati ya rufaa ya TFF kupinga uamuzi wa kusimamishwa kugombea uongozi ndani ya klabu ya simba.

Wambura alisema amekua mwanachama hai wa klabu ya simba tena aliye hai na alishiriki kuiweka madarakani tume hiyo ya uchaguzi iliyomsimamisha kugombea uraisi wa TFF, wakati upande wao tume kuendelea kudai kutomjua Wambura kama mwanachama hai ndani ya klabu.

AC MILLAN WAMTIMUA RASMI KOCHA WAO CLARENCE SEEDORF

Klabu ya soka ya nchini Uitaliano ya Ac milan imemtimua rasmi kocha wake Clarence Seedorf na kumpa kibarua hicho aliyekuwa mchezaji wake wa zamani philipo Inzag ambaye alikuwa akitumika kama kocha wa timu B ya Ac Milan.

Ac Milan wamefikia uamuzi huo baada ya mwenendo wa kocha Seedorf kutokuwa mzuri tangu alipopokea timu kutoka kwa kocha Massimilliano ambaye pia alitimuliwa na klabu hiyo baada ya mwenendo wa timu kuwa mbovu.

habari za kutimuliwa seedorf zimetolewa na klabu ya Ac milan kupitia mtandao wao rasmi ambao  ulithibitisha uteuzi wa kocha Inzaghi kuwa kocha mkuu ambaye amesaini mkataba wa takribani miaka miwili.

Mholanzi Seedorf amekua na mazingira magumu ndani ya klabu hiyo tangu alipopokea toka kwa kocha Massimiliano na kuhisababishia timu kupata matokeo mabovu hadi mwisho wa msimu.

Tuesday, 3 June 2014

TAZAMA VIDEO YA MCHEZA MIELEKA BATISTA AKITANGAZA KUJITOA WWE

Batista alifikia uamuzi huo mara baada ya kunyimwa pambano na The shield. na baadae kuposti kwenye ukurasa wake wa twitter maneno yaliyosomeka i dont need WWE, WWE needs me, akimaanisha sihitaji WWE, WWE inanihitaji.

LIVERPOOL MBIONI KUMNASA ADAM LALLANA

Liverpool mbioni kumnasa kiungo wa Southampton Adam Lallana baada ya klbu ya Tottenham kujitoa kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka.

Awali ilisemekana lallana angejiunga na Tottenham kumfuata kocha wake aliyekuwa akimfundisha Southampton aliyepata kibarua hicho siku si nyingi klabuni hapo.

Liverpool tayari walishaongeza dau la kiasi cha paundi millioni 25 kutoka ile ya awali paundi millioni 20 lakini Southampton wanaonesha kusimamia msimamo wao ule ule wakuitaji paundi millioni 30.

Kwa upande wake mchezaji Adam Lallana anonesha kuzidi kuvutiwa zaidi na Liverpool mara baada ya mchezaji mwenzie walie kuwa nae southampton kujiunga na Liverpool yaani Rickie Lambert, hii imezidi kumvuta zaidi Lallana ndaani ya Anfield .



Lallana ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa anapo cheza katikati kama kiungo mshambuliaji na anaonekana kuwa msaada mkubwa kwa liverpool pale atakapo kuwa nyuma ya washambuliaji hatari wa Liverpool yaani Suarez na Sturridge.

Sunday, 1 June 2014

VITAZAME BAADHI YA VITUKO VYA KOCHA ARSENE WENGER

https://www.youtube.com/watch?v=2EIMBuORLpc

LIVERPOOL WAONGEZA DAU KUMSAJILI LALLANA

Klabu ya soka ya Liverpool ya nchini Uingereza iliyopo mbioni kumsajili kiungo wa Southampton Adam Lallana imeongeza dau kiasi cha paundi milioni 5 ilikunasa saini ya mchezaji huyo baada ya dau la awali kukataliwa.

Mwanzoni Liverpool walitenga kiasi cha paundi milioni 20 ambazo zilikataliwa na klabu ya Southampton kama dau la kumwachia kiungo wao. Tayari Liverpool washafikia makubaliano ya kumchukua beki mwingine wa klabu hiyo Rickie Lambert ambaye tayari keshafanyiwa na vipimo vya kiafya.

Licha ya Liverpool kutangaza dau hilo bado Southampton wanaoneka kusimamia msimamo wao wa paundi milioni 30 ndo wamwachie kiungo huyo aliyekua moja ya chachu ya timu kumaliza nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi msimu uliomalizika.

kocha Brenden Rogers anaonesha wazi wazi kumhitaji kiungo huyo ili kuimarisha timu yake ya msimu ajao akipewa sapoti na baadhi ya viongozi wa timu, bila shaka inaonesha watafikia muafaka kabla ya kombe la Dunia kukamilika.

Friday, 30 May 2014

DAVID DEGEA ANAMSHAWISHII CESC FABREGAS KUHAMIA MAN U

Goli kipa wa klabu ya Manchester United Mhisipania David Degea amesema ameanza kumshauri Mhisipania mwenzie Cesc Fabregas kujiunga nae katika klabu ya Man u ya nchini Uingereza.

Fabregas ambaye ni mchezaji wa klabu ya Barcelona kumekua na taarifa kuwa anahitaji kuhama badada ya msimu huu uliomalizika.

"Nimekua nikimshawishi Fabregas kujiunga na Man u". alisikika akisema Goli kipa huyo wa Man u alipokua kwenye mahojiano na kituo kimoja cha luninga nchini Hispania.

Degea anakutana na wakati kumgumu kumshauri Fabregas kuiacha klabu yake ya Hispania FC BARCELONA kujiunga na klabu yake ya Man u kwani msimu uliopita aliyekua kocha wa Man u David Moyes Tayari alishashindwa.

Kocha wazamani wa Fabrigas ambaye ndiye kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amekua akimhitaji kumrudisha kikosini, hivyo ni upinzani mkubwa watakao kutana nao Man u kumshawishi kujiunga nao chini ya kocha wao mpya Van Gaal.

Ushawishi wa Degea unawapa nafasi kubwa Man u kumtwaa Febregas kutokana na ukweli kuwa klabu ya Arsenal inao viungo wa katikati tayari, kama Ozil, Wilshire na Cazorla, ambao wataleta swali gumu la wapi au nafasi gani Fabregas atacheza?

SAGNA ATANGAZA KUIACHA ARSENAL MSIMU UJAO

Beki wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Bacary Sagna ametangaza rasmi kuiacha klabu hiyo ya jijini London nchini Uingereza.

akizungumza na gazeti la French newspaper L’Equipe la nchini kwao alisema amefikia uamuzi wa kuiacha klabu ya Arsenal aliyoichezea kwa takribani miaka 10 baada ya kutofikia muafaka wa mazungumzo kati yake na klabu.

Vilabu kama Liverpool na Man city vimekua vikimuhitaji beki huyo na Man city wao wakifikia mbali kwa kumuaidi donge nono endapo atjiunga nao msimu ujao wa ligi kuu ya nchini Uingereza.

"Sio siri tena kwa sasa ntaondoka Arsenal, nimejaribu niwezavyo lakini sijafanikiwa kutokana na mazungumzo baina yangu mimi na klabu kutoenda sawa, napokea simu nyingi nikihitajika timu kadha wa kadha mpaka zinaniumisha kichwa, lakini nategemea kufikia muafaka kabla ya kwenda kombe la Dunia". Alisema Sagna

Kwa upande wao Arsenal watamkosa kwa kiasi kikubwa beki huyo kwani kwa kipindi chote alichokuepo klabuni hapo amekua ni msaada mkubwa kwa klabu hiyo ya jijini London.

DI MARIA ALIA NA REAL MADRID KUTAKA KUMUUZA TOTTENHAM

Mshambuliaji wa pembeni (winga) wa Real madrid Angel Di maria amelia na kilabu yake baada ya kuzuka  uvumi kuwa anataka kuuzwa kwenye klabu ya soka ya nchini Uingereza ya Tottenham.

"Inaumiza sana kama mchezaji siku zote unajitahidi kufanya uwezavyo kuisadia kilabu yako lakini mwisho wa siku unasikia kwamba kunampango wakuuzwa Tottnham". alilalamika Di maria wakati akizungumza na Gazeti la Marca.

Di maria kwa sasa ni mchezaji aliye katika kiwango cha juu kutokana na kuonyesha uwezo wake katika michezo mbali mbali ya Real Madrid ukiwemo dhidi ya wapinzani wao Barcelona na ule wa fainali ya ligi ya mabingwa ulaya yaani UEFA.

Msimu iliopita alikua ni mchezaji aliyetegemewa kuhama Real Madrid lakini mwisho wa siku hakuwa yeye kwani tulishudia kuhama kwa mchezaji Mesuit Ozil kuelekea Arsenal na Di maria akibaki kikosini,.

Di Maria amebaki kusema kuwa mstakabali wa maisha yake ndani ya Santiago Bernabeu upo chini ya Real Madrid, endapo wataendelea kumhitaji na kumtumia kama mchezaji wao ama watahamua kumuuza.

"Nilizungumza na kocha nikamweleza nahitaji kuendelea kuwepo pia na yeye alisema ananihitaji uwepo wangu, aliniambia ananitegemea sasa kazi ilibaki kwangu kama mchezaji". alisisitiza Di maria.

Pia Di maria akusita kumsifia kocha wake Ancheloti nakusema kuwa, kajifunza mengi chini ya ualimu wake na alifanya maamuzi sahihi kuendelea kubaki ndani ya Real Madrid.

Alisisitiza kuwa afikilii baadae yake kwa sasa kwani ipo chini ya kilabu yake ya Real Madrid licha ya kukubali uwepo wa timu kubwa zinazo muhitaji lakini awezi sema chochote akisubiri kilabu kusema kama inahitaji aendelee kuwepo ama aondoke.

BALOTELLI AWABEZA WAINGEREZA KOMBE LA DUNIA BRAZIL

Mshambuliaji wa timu ya taifa  ya Italia Mario Ballotelli amekibeza kikosi cha kocha Roy Hudgson kuwa hakiogopeki kombe ladunia mwaka huu na pia hategemei kuwa wapinzani wakubwa na washindani kwenye michuano hiyo.

akihojiwa na gazeti la Daily Mail baloteli alisema afikilii kama timu ya taifa ya Uingereza kuwa mpinzani mkubwa na mshindi wa kombe la Dunia mwaka huu licha ya kuwa na wachezaji wazuri.

"Sifikilii Uingereza kuwa washindi wa kombe la Dunia mwaka huu licha ya kuwa na wachezaji wazuri lakini si washindani wa Italia". Alinukuliwa Balotelli.

aliendelea kusema kuwa hamaanishi kuwa Italia ni Timu bora katika kombe hili la Dunia bali wanawachezaji wenye morali ya kucheza na kuishangaza Dunia kuliko kikosi cha waingereza. alendelea kubeza kuwa wanawachezaji ambao walishashinda kombe la Dunia wakati waingereza hawana.

Uingereza watacheza na Italia mechi yao ya kwanza tarehe 14 Juni kabla hawajacheza na Uruguay na Kosta rika katika michezo itakayofuatia ya kundi D. Waingereza wacheza na Italia akikumbuka kuondoshwa na hao Waitaliano katika michuano ya EURO 2012 kwa mikwaju ya penati baada ya kudroo 0-0 kwenye hatua ya makundi.

 Balotelli alimaliza kwa kusema Waingereza wanawachezaji wawili au watatu wakuogopwa kwenye kombe la Dunia lakini sio kikosi kizima cha Uingereza. wanajiamini na wana uhakika wa kushinda michezo yao.
source sky sport

LIVERPOOL MBIONI KUMNASA BEKI WA KUSHOTO WA SEVILLA ALBERTO MORENO

Kilabu ya soka ya LIVERPOOL ipo mbioni kumnasa beki wa kushoto wa timu ya sevilla ya huko hisipania.

LIVERPOOL wametoa kiasi cha paundi milioni 20 kama ofa ya kumnsa beki huyo ambapo wameweka mezani tayari ofa ya kiasi cha paundi 16 milioni na kumtoa mchezaji wao SUSO kwa mkopo kwenye kilabu ya sevilla.

LIVERPOOL walimaliza msimu wa ligi kuu ya uingereza wakiwa wa pili nyuma ya MAN CITY walioibuka vinala wa ligi hiyo.

kwa sasa kocha wa LIVERPOOL anamtumia Flanagan kama beki wa kushoto ambaye kimchezo anaonekana kuwa bora zaidi na imara upande wa kulia, sasa ujio wa MORENO ndani ya kikosi cha BRENDEN ROGERS utakua msaada mkubwa kwa msimu ujao ambao wanaitaji mafanikio zaidi kuliko ya msimu huu.

Mhisipania MORENO ameweza kufunga magoli matatu kati ya magoli 29 waliyoyapata kilabu ya sevilla msimu huu wakimaliza katika nafasi ya tano ya ligi ya hisipania yaani LA LIGA.

Moreno ni mmoja wa wachezaji mbadala wa kikosi cha Vicente Del Bosque kinachojifua kujiandaa na kombe la Dunia linaloanza mwezi juni huko Brazil. endapo Moreno atapata nafasi ya kuichezea timu ya taifa na kufanya vizuri basi ataipa mwanya timu yake ya Sevilla kuongeza dau la kumuuza.
Moreno anasifika kwa kasi na uwezo mkubwa wa kukimbia na mpira kushambulia lakini pia bila kuyasahau majukumu yake ya ukabaji.

Anaonekana kuwa msaada mkubwa kwa Liverpool kwa ataongeza nguvu safu ya ulinzi na aina yake ya uchezaji ni upendeleo wa kocha wa liverpool Brenden Rogers ambaye kikosi chake kinafunga sana na kuruhusu pia kufungwa goli nyingi pia kutokana na safu ya ulimzi kulega kulega.