Mwenyekiti wa klabu ya soka ya Mbeya City Bw Musa Mapunda amesma hakuna miujiza siku zote katika mchezo wa mpira wa miguu. aliyasema hayo kufuatia mafanikio makubwa waliyoyapata klabu ya Mbeya City kwenye ligi ya Tanzania Bara mwaka 2013/2014, licha ya kutobeba ubingwa.
Mbeya City ni klabu iliyopanda daraja msimu uliopita nakufanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu ya ligu kuu ya Tanzania bara, na kuzipiku timu kubwa kama Simba, Kagera sugar na Mtibwa.
Alisema Mpira wa miguu hauna miujiza zaidi ya uongozi mzuri na wenye malengo ya mafanikio ndani ya klabu na kubeza timu kubwa kuwa migogoro wliyonayo ndani ya vilabu vyao ndo chanzo cha timu timu hizo kubwa kuvurunda kisoka.
Aliendelea kusema kuwa kinacho tokea hivi sasa ni watu wenye uchu na madaraka kugombea nafasi ndani ya vilabu vyao ili kutimiza malengo yao binafsi bila kujali maslahi ya timu, kitu ambacho ni makosa makubwa kwa mwenendo wa soka la timu na taifa kwa ujumla.
Kwa sasa Mbeya City wamepata uzamini mkubwa toka kampuni ya kuuza matairi ya magari ya Binslum, Ambayo inakadiliwa kuweka kiasi cha shilingi milioni 360 kwenye mkataba wa udhamini kati ya kmpuni hiyo yenye makazi yake jijini Dar es salaam na klabu hiyo ya jijini Mbeya.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Mbeya City aliendelea kusema kuwa soka ni biashara na ili ufanikiwe unahitaji kuwekeza kiasi kikubwa na kusema timu yao inajipanga vizuri kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania bara.

No comments:
Post a Comment