Klabu ya soka ya nchini Uitaliano ya Ac milan imemtimua rasmi kocha wake Clarence Seedorf na kumpa kibarua hicho aliyekuwa mchezaji wake wa zamani philipo Inzag ambaye alikuwa akitumika kama kocha wa timu B ya Ac Milan.
Ac Milan wamefikia uamuzi huo baada ya mwenendo wa kocha Seedorf kutokuwa mzuri tangu alipopokea timu kutoka kwa kocha Massimilliano ambaye pia alitimuliwa na klabu hiyo baada ya mwenendo wa timu kuwa mbovu.
habari za kutimuliwa seedorf zimetolewa na klabu ya Ac milan kupitia mtandao wao rasmi ambao ulithibitisha uteuzi wa kocha Inzaghi kuwa kocha mkuu ambaye amesaini mkataba wa takribani miaka miwili.
Mholanzi Seedorf amekua na mazingira magumu ndani ya klabu hiyo tangu alipopokea toka kwa kocha Massimiliano na kuhisababishia timu kupata matokeo mabovu hadi mwisho wa msimu.

No comments:
Post a Comment