Monday, 21 July 2014

ROONEY APANAIA KUMSHANGAZA KOCHA WAKE VAN GAL

Mchezaji wa klabu ya soka ya Manchester United Wayne Rooney  amesema yupo tayari kumshangaza kocha wake mpya Van gal baada ya kuanza kufanya nae mazoezi.

Rooney amesema yupo tayari kufanya kila awezalo mazoezini ili kumuonesha uwezo wake kocha huyo mpya kutoka nchini Uholanzi.

Van gal anatarajiwa kutangaza kapteni wake klabuni hapo wakati wowote ambapo macho mengi yakiwa ni kwa Van persie ama Rooney.

Van persie amekua kepteni wa timu ya taifa chini ya kocha huyo huyo mholanzi ambaye amekifikisha kikosi nafasi ya tatu katika mashindano yaliyokamilika ya kombe la Dunia huko nchini Brazil.

Rooney pia anapewa nafasi kubwa kutokana na ukweli kuwa amekuwa na ushawishi mkubwa ndani ya klabu hiyo na nikiongozi mzuri wa wachezaji wenzake.

Rooney amesema huu ndo wakati wa kumuonesha kocha kile walichonacho wachezaji ili kumrahisishia upangaji wa kikosi cha Man U.

Wachezaji wengine pia kama Mata wanasema wamejiandaa vizuri kutetea klabu ya licha ya kuwa na matokeo magumu katika timu ya taifa iliyoondolewa mapema kwenye mashindano ya kombe la Dunia huko Brazil.

No comments:

Post a Comment